Vipengele vya Kanisa-MS

Kila kitu kanisa lako linahitaji, ndani ya mfumo mmoja.

Hii ndiyo orodha kamili — kuanzia daftari la washirika hadi risiti ya sadaka ya Jumapili, kuanzia WhatsApp hadi ripoti ya mwaka. Hakuna cha kusakinisha: fungua kwenye simu au kompyuta.

Plan kuanzia TZS 25,000 kwa mwezi · Tunatumiwa na makanisa 22+ Tanzania
49vipengele
7maeneo ya maisha ya kanisa
2Kiswahili + English
∞washirika, bila kikomo
Watu Ibada Fedha Mawasiliano Kiroho Ripoti Mfumo Portal
Watu

Washirika, familia na huduma

Kila mshirika, familia, idara na kiongozi mahali pamoja — pamoja na historia yake yote.

vipengele 9
Washirika

Profaili kamili yenye picha, simu, familia na nafasi za uongozi. Tafuta kwa jina au namba papo hapo.

Pakia kwa Excel

Una orodha ya zamani? Ipakie mara moja — mfumo unaonyesha safu zenye makosa kabla ya kuhifadhi.

Mshirika ajisajili mwenyewe

Link na poster ya QR ya kanisa lako. Mshirika anajaza fomu kwenye simu yake, nawe unaidhinisha.

Fomu mnayoiunda

Ongezeni maswali yenu kwenye fomu ya usajili — jumuiya, kwaya, kazi — bila kuhitaji programmer.

Wageni

Mgeni akijisajili anapokea SMS ya karibu kiotomatiki, na anabadilishwa kuwa mshirika kwa bonyeza moja.

Idara

Vijana, wanawake, kwaya — kila idara na washirika wake, sadaka zake na matumizi yake.

Zones na Shemasi

Mgawanyo wa kijiografia wa kanisa, na kufuatilia kazi ya kichungaji na ya ushemasi.

Uongozi

Wachungaji na viongozi, pamoja na kalenda ya majukumu yao.

Contacts

Wageni wa semina, wazazi, wachangiaji — namba zao kwa CSV, bila kuchanganywa na washirika.

Ibada

Ibada na mahudhurio

Mahudhurio yanahesabiwa yenyewe — kwa QR mlangoni, au kwa hesabu ya jumla.

vipengele 6
Check-in kwa QR

QR moja ya kudumu kwa kila tawi. Ibada inachaguliwa yenyewe, na check-in inakubalika wakati wa ibada pekee.

Ratiba zinazojirudia

Weka mara moja — Jumapili, Jumatano, Ijumaa. Mfumo unatengeneza ibada za mwaka mzima wenyewe.

Mahudhurio live

Skrini inayoonyesha waliokwisha kuingia kwa muda halisi, wakati ibada inaendelea.

Hesabu ya jumla

Kwa ibada zisizo na QR: wanaume, wanawake, watoto na wageni — kwa sekunde chache.

Vituo vingi vya ibada

Kila mahali ibada inafanyika lina QR yake ya check-in na ratiba yake — mahudhurio ya kila kituo yanajulikana.

Matukio ya umma

Semina na mikutano kwenye portal, ukurasa wa umma, na widget ya kubandika kwenye website yenu.

Jumapili moja na Kanisa-MS

Kuanzia ukumbusho hadi ripoti — bila makaratasi

  1. Jmos 18:00SMS iliyopangwa inamkumbusha kila mshirika ibada ya kesho.
  2. Jpili 08:30Washirika wanascan QR mlangoni — check-in iko wazi wakati wa ibada tu.
  3. 10:00Ibada inarushwa mubashara ndani ya portal ya mshirika.
  4. 11:30Mhazini anarekodi sadaka; mtu wa pili anathibitisha, na risiti zinatoka.
  5. 13:00Mchungaji anaona mahudhurio na mapato kwenye dashboard.
  6. JtatuWageni wameshapata SMS ya karibu — na wako kwenye orodha ya ufuatiliaji.
Fedha

Sadaka, zaka na matumizi

Kila shilingi ina risiti, mthibitishaji na historia — hakuna kinachopotea kimya kimya.

vipengele 9
Sadaka, zaka na ahadi

Rekodi kila sadaka kwa aina yake. Risiti ya PDF inatengenezwa papo hapo, na inaweza kutumwa tena.

Mtu wa pili anathibitisha

Aliyerekodi sadaka hawezi kuithibitisha mwenyewe — mtu mwingine anahakiki kabla haijahesabiwa.

Kubatilisha, si kufuta

Rekodi iliyokosewa inabatilishwa kwa sababu iliyoandikwa, na inabaki kwenye historia.

Asilimia ya makao makuu

Weka asilimia ya kila aina ya sadaka inayopelekwa jimboni — mfumo unaonyesha kilichokusanywa, kilichopelekwa na salio.

Fundraising

Kampeni zenye lengo, ahadi za washirika, na maendeleo yanayoonekana moja kwa moja.

Matumizi yenye idhini

Katibu anaomba, mchungaji anaidhinisha — kila hatua imeandikwa kwenye audit trail.

Statement ya mwaka

Kila mshirika anapata taarifa ya sadaka na mahudhurio yake — inaweza kutumwa yenyewe tarehe mliyochagua.

Kutoa kwa simu

Mshirika au mtazamaji wa live anafungua link ya kanisa (…/toa), anaweka PIN — pesa inaingia kwenye akaunti ya kanisa (Snippe, Selcom, M-Pesa au Lipa Namba) na risiti inamfikia papo hapo.

Tunawafungulia malipo ya mtandaoni — bure

Tunawaongoza kufungua akaunti ya Snippe hatua kwa hatua: washirika wanatoa kwa M-Pesa, Airtel Money, Mixx, Halotel au QR. Msaada wetu ni bure; Snippe inatoza 2.5% kwa kila malipo.

Mawasiliano

SMS na WhatsApp

Ujumbe unafika kwa mtu sahihi, kwa jina la kanisa lako — na majibu yake hayapotei.

vipengele 7
SMS kwa makundi

Tuma kwa washirika wote, idara, zone au kundi lako — kwa sender ID ya kanisa iliyoidhinishwa na TCRA.

SMS zilizopangwa

Andika leo, itumwe Jumamosi jioni. Mfumo unatuma wenyewe muda ukifika.

WhatsApp rasmi

Namba ya kanisa kwenye WhatsApp Business rasmi (Meta). Tuma taarifa, risiti na matangazo ya picha.

WhatsApp Inbox

Mshirika akijibu, ujumbe unafika kwenye inbox ya kanisa — na mhusika anapata SMS ya kumjulisha.

Matangazo yenye vitufe

Tangazo lenye vitufe kama "Nitahudhuria" au "Sitaweza" — majibu yanahesabiwa yenyewe.

Mshirika kwa WhatsApp

Mshirika anaandika "sadaka", "ratiba" au "biblia" kwenye namba ya kanisa na anajibiwa papo hapo.

Salio la ujumbe

Nunueni SMS na WhatsApp credits ndani ya Billing kwa idadi mnayoihitaji — invoice inatengenezwa papo hapo.

Kiroho

Maombi, Neno na ibada mubashara

Kanisa linaendelea katikati ya wiki — kwenye simu ya kila mshirika.

vipengele 4
Mifungo ya maombi

Mfungo wa siku 21, 7, 3 au moja. Maombi ya kila siku yanatumwa SMS/WhatsApp, na mshirika anathibitisha "Nimeomba".

Mpango wa kusoma Biblia

Ratiba ya kusoma Biblia ya kanisa lenu — mshirika anaandika "biblia" kwenye WhatsApp na anapata somo la leo.

Matangazo ya wiki

Weka matangazo ya Jumapili mara moja — washirika wanayapata kwenye WhatsApp.

Ibada mubashara

Unganisha YouTube, Facebook Live, redio au TV ya kanisa — washirika wanatazama ndani ya portal yao.

Portal ya mshirika

Kila mshirika ana akaunti yake — bila password

Mshirika anafungua portal kwenye simu yake, anaandika namba yake na msimbo wa SMS. Viongozi wanaacha kujibu maswali yale yale kila wiki.

  • Kuingia kwa msimbo wa SMS
  • Sadaka na risiti zake, wakati wowote
  • Rekodi ya mahudhurio yake
  • Ratiba ya ibada na matukio yajayo
  • Kutazama ibada mubashara
  • Mifungo ya maombi — "Nimeomba"
  • Kusasisha taarifa zake mwenyewe
NM
Neema Mushi
Anachoona mshirika
Sadaka 2026TZS 480,000
Ibada alizohudhuria38 / 42
Ibada ijayoJpili 09:00
MfungoSiku 5 kati ya 21
Ripoti

Uongozi na ripoti

Mchungaji anaona hali ya kanisa kwa dakika moja, na kila kiongozi anaona eneo lake tu.

vipengele 7
Dashboard

Muhtasari wa kanisa kwa mtazamo mmoja, pamoja na dokezo la wiki — mfano washirika wanaohitaji kufuatiliwa.

Ripoti za PDF na Excel

Fedha, mahudhurio, washirika, idara na ripoti ya mwaka — tayari kwa kikao cha kamati.

Ripoti za idara na zone

Viongozi wa idara, zone na shemasi wanatuma ripoti; mchungaji na katibu wanazipitia sehemu moja.

Portal za viongozi

Kiongozi wa idara au zone anaona watu, sadaka na matumizi ya eneo lake tu.

Growth
Matawi yenye portal yao

Kila tawi lina anwani yake, viongozi, washirika, sadaka na matumizi yake. Kanisa mama linaona matawi yote pamoja na linaweza kuingia kuhariri tawi lolote.

Majukumu 13

Admin, mchungaji, mhazini, katibu, viongozi wa idara na zone — kila mmoja anaona anachostahili.

Audit trail

Kila kitendo muhimu kinaandikwa: nani, lini, na nini kilibadilika.

Mfumo

Usalama na urahisi

Data ya kanisa lako ni mali yako — imetengwa, iko salama, na inafunguka popote.

vipengele 7
Database yenu peke yenu

Kila kanisa lina database yake tofauti — data yenu haichanganyiki na ya kanisa lingine.

Kuingia salama

Washirika wanaingia kwa msimbo wa SMS; viongozi kwa akaunti zao binafsi.

Kiswahili na English

Kila mtumiaji anachagua lugha yake — mfumo mzima, ripoti na portal.

Kama app kwenye simu

Isakinishe kwenye skrini ya simu bila Play Store, na utumie hali ya usiku (dark mode).

Growth
Domain yenu wenyewe

Kila kanisa linapata anwani kama mlimawabaraka.kanisa.or.tz — au domain yenu kama ms.mlimawabaraka.or.tz. Mkilipia Growth kwa mwaka, tunawasajilia domain bure.

Pata kamisheni

Kanisa likialika kanisa jingine linapata kamisheni — inayoweza kulipia SMS au usajili.

Msaada

Tiketi za msaada ndani ya mfumo, na timu yetu kwenye WhatsApp.

Hakuna kipengele kinacholingana. Jaribu neno lingine, au tuulize WhatsApp.

Vipengele vyenye alama ya Growth vinakuja na plan ya Growth. SMS na WhatsApp zinatumia salio la ujumbe mnalonunua kwenye Billing. Linganisha plan →

Jaribu kila kipengele bure kwa siku 30

Hakuna kadi, hakuna malipo sasa. Tunakusaidia kuingiza washirika wako.