Washirika, familia na huduma
Kila mshirika, familia, idara na kiongozi mahali pamoja — pamoja na historia yake yote.
Profaili kamili yenye picha, simu, familia na nafasi za uongozi. Tafuta kwa jina au namba papo hapo.
Una orodha ya zamani? Ipakie mara moja — mfumo unaonyesha safu zenye makosa kabla ya kuhifadhi.
Link na poster ya QR ya kanisa lako. Mshirika anajaza fomu kwenye simu yake, nawe unaidhinisha.
Ongezeni maswali yenu kwenye fomu ya usajili — jumuiya, kwaya, kazi — bila kuhitaji programmer.
Mgeni akijisajili anapokea SMS ya karibu kiotomatiki, na anabadilishwa kuwa mshirika kwa bonyeza moja.
Vijana, wanawake, kwaya — kila idara na washirika wake, sadaka zake na matumizi yake.
Mgawanyo wa kijiografia wa kanisa, na kufuatilia kazi ya kichungaji na ya ushemasi.
Wachungaji na viongozi, pamoja na kalenda ya majukumu yao.
Wageni wa semina, wazazi, wachangiaji — namba zao kwa CSV, bila kuchanganywa na washirika.
Ibada na mahudhurio
Mahudhurio yanahesabiwa yenyewe — kwa QR mlangoni, au kwa hesabu ya jumla.
QR moja ya kudumu kwa kila tawi. Ibada inachaguliwa yenyewe, na check-in inakubalika wakati wa ibada pekee.
Weka mara moja — Jumapili, Jumatano, Ijumaa. Mfumo unatengeneza ibada za mwaka mzima wenyewe.
Skrini inayoonyesha waliokwisha kuingia kwa muda halisi, wakati ibada inaendelea.
Kwa ibada zisizo na QR: wanaume, wanawake, watoto na wageni — kwa sekunde chache.
Kila mahali ibada inafanyika lina QR yake ya check-in na ratiba yake — mahudhurio ya kila kituo yanajulikana.
Semina na mikutano kwenye portal, ukurasa wa umma, na widget ya kubandika kwenye website yenu.
Kuanzia ukumbusho hadi ripoti — bila makaratasi
- Jmos 18:00SMS iliyopangwa inamkumbusha kila mshirika ibada ya kesho.
- Jpili 08:30Washirika wanascan QR mlangoni — check-in iko wazi wakati wa ibada tu.
- 10:00Ibada inarushwa mubashara ndani ya portal ya mshirika.
- 11:30Mhazini anarekodi sadaka; mtu wa pili anathibitisha, na risiti zinatoka.
- 13:00Mchungaji anaona mahudhurio na mapato kwenye dashboard.
- JtatuWageni wameshapata SMS ya karibu — na wako kwenye orodha ya ufuatiliaji.
Sadaka, zaka na matumizi
Kila shilingi ina risiti, mthibitishaji na historia — hakuna kinachopotea kimya kimya.
Rekodi kila sadaka kwa aina yake. Risiti ya PDF inatengenezwa papo hapo, na inaweza kutumwa tena.
Aliyerekodi sadaka hawezi kuithibitisha mwenyewe — mtu mwingine anahakiki kabla haijahesabiwa.
Rekodi iliyokosewa inabatilishwa kwa sababu iliyoandikwa, na inabaki kwenye historia.
Weka asilimia ya kila aina ya sadaka inayopelekwa jimboni — mfumo unaonyesha kilichokusanywa, kilichopelekwa na salio.
Kampeni zenye lengo, ahadi za washirika, na maendeleo yanayoonekana moja kwa moja.
Katibu anaomba, mchungaji anaidhinisha — kila hatua imeandikwa kwenye audit trail.
Kila mshirika anapata taarifa ya sadaka na mahudhurio yake — inaweza kutumwa yenyewe tarehe mliyochagua.
Mshirika au mtazamaji wa live anafungua link ya kanisa (…/toa), anaweka PIN — pesa inaingia kwenye akaunti ya kanisa (Snippe, Selcom, M-Pesa au Lipa Namba) na risiti inamfikia papo hapo.
Tunawaongoza kufungua akaunti ya Snippe hatua kwa hatua: washirika wanatoa kwa M-Pesa, Airtel Money, Mixx, Halotel au QR. Msaada wetu ni bure; Snippe inatoza 2.5% kwa kila malipo.
SMS na WhatsApp
Ujumbe unafika kwa mtu sahihi, kwa jina la kanisa lako — na majibu yake hayapotei.
Tuma kwa washirika wote, idara, zone au kundi lako — kwa sender ID ya kanisa iliyoidhinishwa na TCRA.
Andika leo, itumwe Jumamosi jioni. Mfumo unatuma wenyewe muda ukifika.
Namba ya kanisa kwenye WhatsApp Business rasmi (Meta). Tuma taarifa, risiti na matangazo ya picha.
Mshirika akijibu, ujumbe unafika kwenye inbox ya kanisa — na mhusika anapata SMS ya kumjulisha.
Tangazo lenye vitufe kama "Nitahudhuria" au "Sitaweza" — majibu yanahesabiwa yenyewe.
Mshirika anaandika "sadaka", "ratiba" au "biblia" kwenye namba ya kanisa na anajibiwa papo hapo.
Nunueni SMS na WhatsApp credits ndani ya Billing kwa idadi mnayoihitaji — invoice inatengenezwa papo hapo.
Maombi, Neno na ibada mubashara
Kanisa linaendelea katikati ya wiki — kwenye simu ya kila mshirika.
Mfungo wa siku 21, 7, 3 au moja. Maombi ya kila siku yanatumwa SMS/WhatsApp, na mshirika anathibitisha "Nimeomba".
Ratiba ya kusoma Biblia ya kanisa lenu — mshirika anaandika "biblia" kwenye WhatsApp na anapata somo la leo.
Weka matangazo ya Jumapili mara moja — washirika wanayapata kwenye WhatsApp.
Unganisha YouTube, Facebook Live, redio au TV ya kanisa — washirika wanatazama ndani ya portal yao.
Kila mshirika ana akaunti yake — bila password
Mshirika anafungua portal kwenye simu yake, anaandika namba yake na msimbo wa SMS. Viongozi wanaacha kujibu maswali yale yale kila wiki.
- Kuingia kwa msimbo wa SMS
- Sadaka na risiti zake, wakati wowote
- Rekodi ya mahudhurio yake
- Ratiba ya ibada na matukio yajayo
- Kutazama ibada mubashara
- Mifungo ya maombi — "Nimeomba"
- Kusasisha taarifa zake mwenyewe
Uongozi na ripoti
Mchungaji anaona hali ya kanisa kwa dakika moja, na kila kiongozi anaona eneo lake tu.
Muhtasari wa kanisa kwa mtazamo mmoja, pamoja na dokezo la wiki — mfano washirika wanaohitaji kufuatiliwa.
Fedha, mahudhurio, washirika, idara na ripoti ya mwaka — tayari kwa kikao cha kamati.
Viongozi wa idara, zone na shemasi wanatuma ripoti; mchungaji na katibu wanazipitia sehemu moja.
Kiongozi wa idara au zone anaona watu, sadaka na matumizi ya eneo lake tu.
Kila tawi lina anwani yake, viongozi, washirika, sadaka na matumizi yake. Kanisa mama linaona matawi yote pamoja na linaweza kuingia kuhariri tawi lolote.
Admin, mchungaji, mhazini, katibu, viongozi wa idara na zone — kila mmoja anaona anachostahili.
Kila kitendo muhimu kinaandikwa: nani, lini, na nini kilibadilika.
Usalama na urahisi
Data ya kanisa lako ni mali yako — imetengwa, iko salama, na inafunguka popote.
Kila kanisa lina database yake tofauti — data yenu haichanganyiki na ya kanisa lingine.
Washirika wanaingia kwa msimbo wa SMS; viongozi kwa akaunti zao binafsi.
Kila mtumiaji anachagua lugha yake — mfumo mzima, ripoti na portal.
Isakinishe kwenye skrini ya simu bila Play Store, na utumie hali ya usiku (dark mode).
Kila kanisa linapata anwani kama mlimawabaraka.kanisa.or.tz — au domain yenu kama ms.mlimawabaraka.or.tz. Mkilipia Growth kwa mwaka, tunawasajilia domain bure.
Kanisa likialika kanisa jingine linapata kamisheni — inayoweza kulipia SMS au usajili.
Tiketi za msaada ndani ya mfumo, na timu yetu kwenye WhatsApp.
Vipengele vyenye alama ya Growth vinakuja na plan ya Growth. SMS na WhatsApp zinatumia salio la ujumbe mnalonunua kwenye Billing. Linganisha plan →
Jaribu kila kipengele bure kwa siku 30
Hakuna kadi, hakuna malipo sasa. Tunakusaidia kuingiza washirika wako.