Miongozo yote
Anza Hapa

Anza Kutumia Kanisa-MS

Hatua za kwanza baada ya kusajili kanisa lako — onboarding wizard, kuingiza washirika, na kuanzisha michango.

1. Kusajili Kanisa Lako

Nenda kanisa.or.tz bonyeza Anza Bure. Jaza jina la kanisa, mkoa, na barua pepe yako. Utapata subdomain yako mwenyewe (mfano kanisalangu.kanisa.or.tz).

2. Onboarding Wizard

Ukiingia mara ya kwanza, utaonana na wizard wa hatua 5:

  • Ongeza maelezo ya kanisa
  • Tengeneza idara za awali (Kwaya, Vijana, n.k.)
  • Tengeneza kanda za fellowship
  • Ongeza viongozi wa kwanza
  • Sanidi njia za malipo

3. Kuingiza Washirika

Nenda Members → Add Member. Unaweza kuingiza mmoja mmoja au ku-upload Excel.

4. Kuanzisha Michango

Bonyeza Contributions → New. Chagua mshirika, tarehe, na kiasi.

Wakati huu, umeanza!