Mfumo wa Kitanzania · Data yako ni mali yako

Simamia Kanisa Lako kwa
Mfumo Mmoja Kamili

Washirika, mahudhurio, sadaka, matumizi, idara, SMS, na ripoti — yote sehemu moja, 100% Kiswahili, na bei nafuu kwa kanisa lolote.

Tunatumiwa na 21+ makanisa Tanzania
Mfano · kanisa lako leo Hai
Mlima wa Baraka Church
Dar es Salaam · washirika 482
Growth
Mahudhurio ya Jumapili 4 zilizopita
438 walihudhuria Jumapili
TZS 3.2M sadaka mwezi huu
1,240 SMS zimefika
+18 washirika wapya
Kila kanisa linapata anwani yake: mlimawabaraka.kanisa.or.tz
21+Modules
13Role Types
100%Kiswahili + English
∞Washirika

Kila Kitu Unachohitaji kwa Kanisa

Mfumo mmoja unaobeba mahitaji yote ya kiutawala — bila kuhamishia data hapa na pale.

Washirika

Profaili kamili na picha, simu, familia, na uongozi. Search ya haraka.

Check-in kwa QR

QR moja ya kudumu kwa kila tawi. Ibada inapickiwa kiotomatiki, na PIN inayoonyeshwa skrini inazuia wasiofika kujiandikisha.

Ratiba Zinazojirudia

Weka mara moja — Jumapili, Jumatano, Ijumaa. Mfumo unatengeneza ibada za mwaka mzima wenyewe.

Sadaka & Zaka

Rekodi sadaka, zaka, michango ya ahadi. Risiti za PDF moja kwa moja.

Matumizi

Approval workflow — secretary anaomba, mchungaji anaaprove, na audit trail.

Idara

Vijana, wanawake, choir — kila idara na portal yake, sadaka na matumizi.

Zones na Shemasi

Mgawanyo wa kijiografia, kufuatilia kazi ya kichungaji na ushemasi.

Portal ya Mshirika

Kuingia kwa OTP — bila password. Mshirika anaona michango, mahudhurio, ratiba na risiti zake, na anaweza kupakua taarifa.

Ibada Mubashara

Unganisha YouTube, Facebook Live, redio au TV ya kanisa — washirika wanatazama ndani ya portal yao.

Mifungo ya Maombi

Mfungo wa siku 21, 7, 3 au moja. Maombi ya kila siku hutumwa SMS/WhatsApp, na mshirika anathibitisha "Nimeomba".

Matukio ya Umma

Semina na mikutano yanaonekana kwenye portal, ukurasa wa umma, na widget ya kubandika kwenye website yako.

Ripoti

Financial, mahudhurio, growth — PDF/Excel exports kwa kasi.

SMS Notifications

Tuma SMS kwa makundi, sender ID yako mwenyewe ya TCRA.

WhatsApp Kanisa

Tuma taarifa, risiti na matangazo ya picha. Mshirika akijibu, ujumbe wake unafika kwenye inbox ya kanisa — si kupotea.

Contacts

Wageni wa semina, wazazi, wachangiaji — ingiza namba zao kwa CSV na uwatumie SMS au WhatsApp bila kuwachanganya na washirika.

Mshirika kwa WhatsApp

Mshirika anaandika "michango", "ratiba" au "biblia" kwenye namba ya kanisa na anajibiwa papo hapo — bila link wala app.

Matangazo & Soma Biblia

Weka matangazo ya wiki na ratiba ya kusoma Biblia ya kanisa lako — washirika wanayapata kwenye WhatsApp.

Fundraising

Campaign zenye lengo, ahadi za washirika, progress tracking live.

Wageni

Mgeni akijisajili anapokea SMS ya karibu kiotomatiki, na anabadilishwa kuwa mshirika kwa bonyeza moja.

Uongozi

Wachungaji, viongozi, na kalenda ya majukumu yao.

13 Roles & Permissions

Admin, pastor, treasurer, secretary, dept/zone leaders na zaidi.

Anza Kwa Dakika 5 — Sio Wiki

1
Sajili Kanisa

Jaza form ya kanisa. Subdomain yako (mfano kanisalako.kanisa.or.tz) inazaliwa moja kwa moja.

2
Ingiza Washirika

Import kutoka Excel au CSV, au kutumia link ya self-registration na QR code.

3
Wezesha Modules

Chagua vipengele unavyohitaji — modules zote ziko kwenye trial yako.

4
Tumia Jumapili

Check-in wa mahudhurio, rekodi sadaka, tuma SMS — yote tayari.

QR Code ya Kujisajili — Bila Kuchapisha

Weka QR code mlangoni mwa kanisa, kwenye group ya WhatsApp, au kwenye poster — washirika wanachemua simu zao, wanajaza fomu, na admin anapokea taarifa moja kwa moja.

  • Hakuna app ya kupakua
  • Hakuna login inayohitajika kwa wenye taarifa mpya
  • Admin ana approval workflow
  • Poster ya A4 imeprint-tayari
QR Sample
Mfano wa QR code
MPYA · KWA WASHIRIKA

Mshirika Anapata Kila Kitu kwa WhatsApp — Bila Link, Bila App

Washirika wengi hawakumbuki password wala hawabofyi link. Sasa wanaandika tu kwenye namba ya WhatsApp ya kanisa, na mfumo unawajibu wenyewe — matangazo ya wiki, somo la Biblia, michango yao, na zaidi.

  • Anaandika "Habari" — au neno moja kama "michango", "ratiba" au "biblia" — na anajibiwa papo hapo, saa yoyote
  • Mfumo unamtambua kwa namba yake ya simu; taarifa zake anaziona yeye tu
  • Swali ambalo mfumo haulielewi linaingia kwenye inbox ya kanisa — mtu halisi anajibu
  • Hakuna credit inayokatwa: mshirika ndiye anayeanza mazungumzo
  • Matangazo na ratiba ya Biblia unaziweka mwenyewe, na unachagua kipi kionekane kwenye menyu
  • Inafanya kazi kwenye namba ya WhatsApp ya kanisa lako — tunakusaidia kuiunganisha
Mshirika anaandika "Habari" au neno moja — jibu linakuja papo hapo
Menyu ya mshirika
Matangazo ya wikiTarehe na saa ya ibada ya Jumapili ijayo, pamoja na matangazo ya wiki hii
Soma BibliaKinachosomwa wiki hii kwa ratiba ya kanisa lako — somo la leo limewekwa alama
Michango yanguJumla ya mwaka huu na mchango wa mwisho
Mahudhurio yanguIbada alizohudhuria mwaka huu, kwa asilimia
Ratiba ya ibadaIbada tano zinazokuja — tarehe, saa na mahali
Taarifa kamiliPDF ya michango ya mwaka inatumwa ndani ya WhatsApp — kwa PIN ukitaka
Taarifa zanguJina, namba ya uanachama, idara na tarehe ya kujiunga
PORTAL YA MSHIRIKA

Kila Mshirika Ana Akaunti Yake — Bila Password

Mshirika anaingiza namba yake ya simu, anapokea msimbo kwa SMS, na yuko ndani. Anaona michango yake, mahudhurio, ratiba ya ibada, na anaweza kupakua risiti na taarifa zake mwenyewe — bila kumuuliza secretary.

  • Kuingia kwa OTP ya SMS — hakuna password ya kusahau
  • Ratiba ya ibada za mwaka mzima — leo, kesho, na wiki zijazo
  • Risiti na taarifa za michango za kupakua wakati wowote
  • Ibada mubashara, redio na TV ya kanisa ndani ya portal
  • Maombi ya mfungo wa siku — anathibitisha "Nimeomba"
  • Anasasisha profaili na namba yake mwenyewe
Msimbo unaisha baada ya dakika chache, na mshirika anaona data yake pekee.
NM
Neema Mushi
Kanisa Langu · MBR-0142
Michango 2026
TZS 480,000
Mahudhurio 2026
38/42
Ratiba ya ibada
Leo
Ibada Kuu ya Jumapili
09:00 · Ukumbi Mkuu
Ibada ya Jioni
18:00 · Ukumbi Mkuu
Nyumbani
Maombi
Tazama
Michango
Profaili
Portal halisi ya mshirika kwenye simu
MALIPO YA MTANDAONI

Malipo ya Mtandaoni kwa Kanisa Lako — Tunawafungulia Bure

Washirika wanataka kutoa kwa simu, lakini kufungua akaunti ya malipo kunachosha. Tunawaongoza hatua kwa hatua kufungua akaunti ya Snippe — usajili, uthibitisho (KYC) na malipo ya kwanza ya majaribio — na hamtulipi chochote kwa msaada huo.

  • Mshirika anapokea ombi la malipo kwenye simu yake na anathibitisha kwa PIN — hakuna kukariri namba za Lipa
  • QR ya kubandika ukumbini, na link ya malipo ya kutuma kwa WhatsApp au SMS
  • Pesa inaingia kwenye akaunti ya kanisa lenyewe — sisi hatushiki pesa zenu
  • Inaunganishwa na portal ya washirika na ukurasa wa /toa — kila mchango unaingia kwenye mfumo wenyewe, na risiti inamfikia mtoaji
1 Tuandikie WhatsApp Tuambie jina la kanisa na mtu atakayesimamia malipo.
2 Tunafungua akaunti pamoja Tunawaongoza kwenye usajili na nyaraka za uthibitisho za Snippe.
3 Mnaanza kupokea Tunafanya malipo ya majaribio pamoja nanyi, kisha mnashiriki link na QR yenu.
Tuombe msaada — bure

Msaada wetu ni bure. Snippe inatoza 2.5% kwa kila malipo yanayofanikiwa — hakuna ada ya kila mwezi.

09:41
Ombi la malipo
Lipa TZS 50,000 kwa Kanisa Langu — Sadaka. Weka PIN kuthibitisha:
••••
GhairiTuma
Malipo yamekamilika — kanisa limepokea TZS 50,000.
M-Pesa Airtel Money Mixx by Yas Halotel QR
Mshirika anathibitisha kwa PIN kwenye simu yake — sekunde chache tu

Bei Nafuu — Bila Kificho

Anza bure siku 30. Hakuna kadi inayohitajika.

Basic

Kwa makanisa ya washirika hadi 250

TZS 25,000 /mwezi

au TZS 250,000/mwaka — okoa miezi 2

  • Modules zote (washirika, sadaka, matumizi, idara)
  • Subdomain yako (slug.kanisa.or.tz)
  • Portal ya mshirika — kuingia kwa OTP
  • Washirika watoe kwa simu kwenye portal — Snippe, Selcom, M-Pesa au Lipa Namba, pesa kwa akaunti ya kanisa
  • Check-in kwa QR na ratiba zinazojirudia
  • Ibada mubashara na mifungo ya maombi
  • Matukio ya umma + widget ya website
  • Backups za wiki
  • Email support
  • SMS notifications (ongeza separately)
Anza Trial Bure
Growth

Kwa makanisa ya washirika zaidi ya 750 au matawi mengi

TZS 120,000 /mwezi

au TZS 1,200,000/mwaka — okoa miezi 2

  • Kila kitu cha Starter, pia:
  • SMS za ukumbusho na za makundi
  • WhatsApp rasmi (Meta Cloud API)
  • Custom sender ID ya TCRA
  • Matawi — kila tawi na portal yake; kanisa mama linaona na kuhariri yote
  • Domain yenu wenyewe — BURE mkilipia kwa mwaka (mfano kanisalenu.or.tz)
  • Ripoti consolidated
  • WhatsApp/Simu support
  • Priority onboarding
Anza Trial Bure

Bei haijajumuisha SMS — kanisa linanunua SMS kwa idadi linayotaka, TZS 18 kwa kila SMS.

Imejengwa kwa Makanisa ya Tanzania

Database ya Kanisa Lako Pekee

Kila kanisa lina DB binafsi — data yako haichanganyiki na ya wengine.

Kiswahili na Kiingereza

UI nzima ipo lugha zote mbili — kuanzia menu hadi ripoti za PDF. Kila mtumiaji anachagua yake.

Malipo ya Simu Ndani ya Mfumo

Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Visa. Push inakuja moja kwa moja simuni — hakuna kuelekezwa nje ya mfumo.

Sakinisha Kama App

Bandika kwenye home screen ya simu — inafunguka kama app, bila kupitia Play Store.

Widget ya Website Yako

Matukio ya kanisa yanaweza kubandikwa kwenye website yako kwa msimbo mmoja — yanajisasisha yenyewe.

Rekodi Haifutwi Kimya

Kila mabadiliko yana audit trail — nani, lini, na alibadilisha nini.

Backup Otomatiki

Data inahifadhiwa kila wiki, na export ya Excel/CSV inapatikana wakati wowote.

Updates za Bure

Vipengele vipya vinaongezwa kila mwezi — kufuatia maoni ya makanisa yanayotumia.

Support kwa WhatsApp

Wasiliana nasi WhatsApp au simu — tunajibu haraka kwa Kiswahili.

Maswali na Majibu

Je, data yangu iko salama?
Ndio. Kila kanisa lina database yake binafsi — data yako haichanganyiki na kanisa lingine. Tunatumia HTTPS na backup kila wiki.
Naweza kuingiza washirika kutoka Excel?
Washirika wanahitaji smartphone?
Mshirika anaingiaje kwenye portal yake?
Je, ratiba ya ibada inajitengeneza?
QR ya check-in inafanyaje kazi?
Tunaweza kuonyesha ibada mubashara?
Naweza kupata data yangu wakati wowote?
Mfumo unatumika kwa madhehebu yote?
Naweza kuwa na matawi?
Nani anamiliki data?
Trial inaisha vipi?
Naweza kuongeza watumiaji wengi?
Mfumo unafanya kazi bila internet?
Una Akaunti Tayari?

Ingia kwa username, email, au simu yako kupitia portal kuu.

Ingia Sasa
au
https:// .kanisa.or.tz
Hujasajili Bado?

Anzisha kanisa lako leo — trial siku 30 bure.

Sajili Kanisa Bure

Hakuna kadi inayohitajika

Tayari Kuanza?

Jiunge na makanisa yanayotumia Kanisa-MS kusimamia washirika, sadaka, na ibada.

Sajili Sasa — Bure Wasiliana WhatsApp
Tuandikie WhatsApp